Bunduki Ft Country Boy – Pesa Lyrics

Bunduki Ft Country Boy - Pesa Lyrics
Bunduki Ft Country Boy – Pesa Lyrics

Bunduki Ft Country Boy – Pesa Lyrics

Yeah yeah, naanza hapo

Mi ndo pesa cheki navyo wasumbua akili
Hawalali kutwa wanakesha kunitafuta midili
Nawapeleka puta mpaka majasho yanatoka
Vikwapa vinawanuka wanipati navyotoka

Adimu kama nini sipatikani kirahisi
Nasakwa hadi porini mimi ni shavu kwa polisi
Ukikamatwa unitoe mimi wengine wananiita rushwa
Nina majina mengi mimi chanzo cha kusaga kutupwa

Waovu wananitumia ni wadhuru watu wema
Na wema wananitumia nami natumika vyema
Moyoni inakuwa faraja, nasahaukisha machungu
Matatizoni ni raha pia ni shida kwenye uchungu
Ili unipate nieke vyema nitunze nikutunze
Usije sema sikusema, kamwe usinipuuze
Wapo wanaonuna wakinikosa visirani haviishi
Usinichokoze utaniponza mi ndo pesa kishawishi

Wananiita pesa, pesa, pesa yeah
Wananiita pesa, pesa, pesa yeah
Wengine waniita money pesa mulla, money
Wengine waniita money pesa mulla, money
Wengine wananiita

Ulizaliwa unanikuta na ukifa unaniacha
Wote wananitafuta na si wote wanaonipata
Nakidhi mahitaji kwenye maamuzi mi ndio jaji
Simpendi mfujaji kurudi kwake sitaraji
Anaenidharau ananitupa anayenidhamini ananiokota
Ukinipoteza utanijuta usingizini utaniota
Nampenda mwenye malengo haijalishi vitendo
Wananitumia kama chambo bila mi hufanyi mambo

Ila ni ngumu kunimiliki sikupi uhakika
Nitakupa vipi kiki na daily unanitafuta
Wengine wananipata kiugumu wengine kirahisi
Wengine wanajihukumu wananihadithia ka hadithi
Pamoja wanaheshimika nikikutosa unadharaulika
Mi mwanako wanakonificha huwezi ona pata picha
Wanaozoea kunikamata wananipata kila saa
Wanaoningojea ni mtata kama Yesu alivyopaa

Wananiita pesa, pesa, pesa yeah
Wananiita pesa, pesa, pesa yeah
Wengine waniita money pesa mulla, money
Wengine waniita money pesa mulla, money
Wengine wananiita

Hakuna saa unauliza kichwa itakuwaje bila pesa
Ukikata tamaa we kwisha ukiogopa maisha unajitesa
Heshima pesa sio maneno siku hizi dhamani kitwa
Haijalishi sherehe ya msumeno nami ndo kila kitu
Ndo nae kupa kiburi usteme kama mate
Nakufanya unakuwa jeuri ukinikosa unakuwa mnyonge
Ujanja kuwa na pesa ongeza utaftaji uwe nazo
Bila malengo wanachekesha juhudi utegwa vikwazo
Ni ndoto kila mtu anaota maisha mazuri mipango
Sio ndoto unaota ukiokota ukishtuka hakuna chako

Ni sumu ni tahadhari silaha kwa binadamu
Ndo pesa hila habari sasa pata ufahamu
Maskini wananitamani niwe karibu yao
Nisiwe mbali dhamani niwe tumaini lao
Matajiri ndo kabisa hawataki niwatoke
Nikiwatoka na wamekwisha wanadhani niko siku zote

Pesa, pesa, pesa yeah
Pesa, pesa, pesa yeah..

Wananiita pesa, pesa, pesa yeah
Wengine waniita money pesa mulla, money
Wengine waniita money pesa mulla, money
Wengine wananiita

Jamie

Call the classic man on +233542793417

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Back to top button