Mbosso – Haijakaa Sawa Lyrics

Mbosso - Haijakaa Sawa
Mbosso – Haijakaa Sawa

Mbosso – Haijakaa Sawa Lyrics

Download : Mbosso – Haijakaa Sawa

(Mocco)

Sasa una nuna nini?
Au unadhani hata mimi napenda
Nishazichoka na mimi
Mboga za majani kila siku mrenda

Siko juu siko chini
Niko nusu sado
Sio wa kumi si sabini
Ngoma ngumu bado

Kama ibada naswali sana
Usiku wa manane tena nafunga na suna
Mambo bado, bado mwana wane
Naona yanazidi kuvuma

Nikirudi na hasira hasira (Nizoee)
Mambo magumu bado bila bila (Niombee)
Nikirudi na hasira hasira (Nizoee)
Mambo magumu bado bila bila (Niombee)

Haijakaa sawa!
Nivumilie ipo siku tutapata
Haijakaa sawa!
Shida na dhiki zitakwisha beiby

Haijakaa sawa!
Kucha na kope make-up utapaka
Haijakaa sawa!
Tutabadili mboga kuku kwa manyama

Chochea kuni kipenzi changu
Asubuhi tumbo likikuminginya
Pokea kidogo changu
Tunywe chai kwa mkate wa kumimina

Akili ikichoka, riziki nikikosa
Najua kwako nitajiliwaza
Kama makosa nivute chumbani
Kununa nuna unajilemaza

Ustahimilivu mnao wachache mno
Jua shida rafiki wa mbivu
Baada ya dhiki mavuno
Kila jema lina maumivu

Na kwenye waliomo tumo
Yarabi salama tupe tulivu
Penzi lisifike kikomo
Iyee iyee

Nikirudi na hasira hasira (Nizoee)
Mambo magumu bado bila bila (Niombee)
Nikirudi na hasira hasira (Nizoee)
Mambo magumu bado bila bila (Niombee)

Haijakaa sawa!
Nivumilie ipo siku tutapata
Haijakaa sawa!
Shida na dhiki zitakwisha beiby

Haijakaa sawa!
Kucha na kopa make-up utapaka
Haijakaa sawa!
Tutabadili mboga kuku kwa manyama

Jamie

Call the classic man on +233542793417

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Back to top button